Personal Websites Babelred
Get your website for free

uondwe shumba vyamboni

0 0 0

Juma Kh Ali

By: Juma Kh Ali. | Created: 05/04/2011 22:54 |
By Juma bin Khamis bin Ali.

Uondwe ni moja kati ya kijiji maarufu na kinachokua kwa kasi katikati ya Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba. Upande wa kaskazini kimepakana kijiji cha Mamoja, kusini Shumba Vyamboni, Mashariki Mgeninje na kwa Upande wa magharibi kipo kijiji cha Jichwa/Bule. Asili ya watu wa Uondwe ni mchanganyiko wa makabila, na kabila maarufu likiwa ni Al rasady, likifuatiwa na Al miskiry, Sukuma, Makonde n.k Takriban watu wote wa Uondwe ni ndugu. Udugu huu ni wa damu, au wa kuoana, au wa ujirani tu. Vijiji maarufu vinavyoijenga Uondwe ni pamoja na Nyumbakati, Kenya, Chanjaani, Ndaambani, Makobeni nk Asilimia 100 ya Wauondwe ni waislamu wenye Madhehebi ya Ibadhi na Sunni. Ipo miskiti minne na Madrasa mbili maarufu kama Tunguu na Suza. Shughuli za uchumi ni Kilimo, ufugaji, Ujenzi, Biashara na michezo imetia nanga kijijini Uondwe. Timu maarufu ikiwa ni Stone fire iliyo daraja la tatu.


Kijiji hichi chenye watu wapatao 300 kipo katika jimbo la tumbe shehia ya Shumba vyamboni. Licha ya kuzungukwa na raslimali nyingi bado raslimali hzo hazijaleta maendeleo ya kweli kijijini hapo

MAJI SAFI NA SALAMA.

Baada ya dhiki faraja. Licha ya kuepo kwa mabomba ya kusafirishia maji kwa takriban miaka kumi na tano huduma ya maji safi na salama haikua ya uhakika. Imechukua kijiji hicho hadi mwaka 2017 kuweza kuonja ladha ya maendeleo ktk sekta ya maji ambapo kufuatia kukamilika kwa kisima cha maji Shumba..Maweni sasa huduma hiyo imekua bwerere, inatakiwa uwe mlipaji mzuri uweze kupata huduma ya maji..

.NISHATI YA UMEME

Baada ya subiri subiri ya nusu karne tokea Uhuru wa nchi yetu mwaka 2015 WAKAAZI WA UONDWE NA VITONGOJI VYAKE WAMEANZA KUTUMIA HUDUMA YA UMEME....

TAARIFA ZAIDI ZINAKUJA

SUALA LA AJIRA


Ukosefu wa ajira kwa vijana ndio tatizo ambalo linatishia ustawi wa kijiji cha uondwe.
ni asilimia 1 pekee ya wanakijiji wenye ajira rasmi za serikali hasa hasa walimu na zaidi ya 70 ya watu wa hapa wamejiajiri wenyewe kupitia kilimo, ufugaji, upigaji tanu na biashara

0 0 0

Juma Kh Ali

By: Juma Kh Ali. | Created: 05/04/2011 22:47 |
Juma Kh Ali ni mzaliwa wa kijiji maarufu Uondwe Nyumbakati wilaya Micheweni Pemba. Amezaliwa 1988. Nimeanza elimu ya madrasa mwaka 1994 na elimu ya Shule mwaka 1996 hapo Shumba Vyamboni. Kwangu mimi dini ndio mfumo sahihi wa matendo na tabia za binadamu. Dini ndio itakayowaongozo binadamu juu ya kufuata njia sahihi za kimaisha. Naamini kua bila dini jamii zitaishi kama wanyama na hakutokua na heshima, nidhamu busara, ustahamilivu na huruma

Kwangu mimi Uislam ndio dini sahihi duniani, kwani ina misingi imara, dira, viongozi na historia ya ukweli. Ndio maana kila kitu kimezungumziwa na kuekwa wazi ndani ya Uislamu, kwa mfano masuala ya matumizi ya mali. Bila uislamu jamii hazitoishi kwa amani, upendo na dhulma na ufisadi vitazidi